Loading...

Ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la 2.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemhukumu mkazi wa kijiji cha Isenegeja kata ya Mwisi, Francis Maganga (54) kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili.

Hakimu wa wilaya, Leonard Nkola alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa cha kumbaka mtoto mdogo ni cha kinyama ambacho hakiwezi kuvumilika katika jamii yetu.

Hakimu Nkola alisema pasipo shaka yoyote ushahidi mahakamani umejitosheleza na mshitakiwa atakwenda jela miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga, Frank Matiku aliiambia Mahakama mbele ya Hakimu Nkola kuwa Mei 25, mwaka huu saa mbili usiku alimkamata kwa nguvu mwanafunzi wa darasa la pili anayesoma shule ya msingi Isenegeja.

Mwendesha Mashitaka aliendelea kuiambia Mahakama kuwa mshitakiwa baada ya kumkamata mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alimvuta kuelekea kwenye nyumba yake na kumbaka huku akimtishia kuwa asipige kelele ya kuomba msaada kwani akifanya hivyo atamchoma kisu.

Matiku alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 130 na 131 cha kwanza cha kanuni ya adhabu sura 16 mapitio ya mwaka 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Baada ya kusomewa shitaka, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na ndipo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi sita mahakamani ambao wote walimtambua mshitakiwa.

ZeroDegree.
Ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la 2. Ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la 2. Reviewed by Zero Degree on 11/17/2016 05:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.