Loading...

Orodha ya wadaiwa sugu wa bodi ya mikopo yaibua mapya.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru. 
Orodha ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imedaiwa kuwataja wanufaika ambao baadhi walishamaliza kulipa madeni yao.

Pia, yapo majina ya watu ambao hawajawahi kuomba mkopo na wengine walisoma nje ya nchi.

Mapema wiki hii Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, alitaja kiasi cha fedha wanazodaiwa wanufaika hao 142,470 kuwa ni Sh2.39 bilioni. Hata hivyo, baadhi ya majina yaliyotolewa katika tovuti ya HESLB ikidai kuwa ni wadaiwa sugu, wametajwa kimakosa.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Orodha ya wadaiwa sugu wa bodi ya mikopo yaibua mapya. Orodha ya wadaiwa sugu wa bodi ya mikopo yaibua mapya. Reviewed by Zero Degree on 11/17/2016 05:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.