Loading...

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro afariki dunia leo.

Fidel Castro amefariki leo akiwa na umri wa miaka 90. Kituo cha televisheni cha serikali nchini humo kimetangaza leo kuwa mwanamapinduzi huyo alifariki saa moja asubuhi.

Kaka yake Castro, Raul Castro ambaye ndiye Rais wa sasa wa Cuba alithibitisha kifo hicho.

Agosti 13 mwaka huu mwanamapinduzi huyo alisherehekea siku yake kuzaliwa akitimiza miaka 90 na katika hotuba yake alitabiri na kusema atakufa siku za karibuni.

Castro aliondoka madarakani miaka 8 iliyopita baada ya kuugua maradhi ya tumbo.


Endela kufuatilia zaidi katika ukurasa huu kupata taarifa zaidi kuhusu kifo cha mwanamapinduzi huyo.

ZeroDegree.
Aliyekuwa Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro afariki dunia leo. Aliyekuwa Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro afariki dunia leo. Reviewed by Zero Degree on 11/26/2016 10:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.