Loading...

Chadema kupata bilioni 13 kwa mwaka kupitia kadi za kieletroniki.

Chadema imetangaza kuwa Januari itaanza kutumia kadi mpya za uanachama za kielektroniki, zitakazoiwezesha kukusanya Sh13.9 bilioni kwa mwaka na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali.

Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika mkoani Morogoro.

Tofauti na Mbowe, viongozi wengine wa chama hicho walioko mikoani ni Edward Lowassa aliyeko Dodoma na Frederick Sumaye ambaye yupo Singida.

Mbowe alisema mfumo huo utasaidia pia kudhibiti baadhi ya viongozi wasio waaminifu, wanaotumia mwanya wa kuuza kadi na kushindwa kuwasilisha fedha kwenye hazina ya chama.

ZeroDegree.
Chadema kupata bilioni 13 kwa mwaka kupitia kadi za kieletroniki. Chadema kupata bilioni 13 kwa mwaka kupitia kadi za kieletroniki. Reviewed by Zero Degree on 11/23/2016 09:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.