Loading...

Habari njema kwa mashabiki wa klabu ya Yanga.

MJUMBE wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Athuman Kihamia, amesema hakuna sababu yoyote inayoweza kuwafanya washindwe kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na kutanguliwa kwa pointi na watani wao wa jadi, Simba.

Simba ipo kileleni mwa ligi hiyo, ikiwa na pointi 35, wakati Yanga ikifuatia kwa kuwa na 33, wakongwe wote hao wa soka nchini wakiwa wamecheza mechi 15 kuhitimisha mzunguko wa kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kihamia, ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, alisema ni ukweli usiopingika kuwa Yanga ina nafasi kubwa ya kutetea kombe msimu huu, kwani ina wachezaji wenye viwango vya kimataifa.

“Naona kabisa kwa hali ilivyo Yanga tuna nafasi kubwa ya kukamata ubingwa msimu huu, ingawaje mahasimu wetu wametuzidi pointi mbili, lakini hiyo siyo sababu ya sisi kushindwa kutetea ubingwa wetu,” alisema Kihamia.

Kihamia aliitaja moja ya sababu iliyowaweka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu mzunguko wa kwanza kuwa ni ubovu wa viwanja kipindi wanacheza ugenini, ikiwemo mechi dhidi ya Mbeya City, ambayo walipoteza kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1, ukiacha ile ya Stand United waliyotoka uwanjani vichwa chini kwa kufungwa bao 1-0.

Kihama alisema, kutokana na matokeo hayo mabaya, kamati nzima ya mashindano itaangalia namna ya kuongeza kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kusaidia ukuta wa Yanga na kusukuma mashambulizi yenye mafanikio kwa timu nzima.

ZeroDegree.
Habari njema kwa mashabiki wa klabu ya Yanga. Habari njema kwa mashabiki wa klabu ya Yanga. Reviewed by Zero Degree on 11/16/2016 12:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.