Loading...

Hatima ya Ester Bulaya kujulikana kesho.

Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya. 
Hatima ya Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya itajulikana kesho wakati Jaji Noel Chocha atakapotoa hukumu.

Awali, hukumu ya shauri hilo namba 01/2015 lililofunguliwa na wapigakura wanne ilipangwa kutolewa Novemba 22, lakini Jaji Chocha amerudisha nyuma kwa siku nne hadi kesho.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alithibitisha jana kuwa badala ya Novemba 22, sasa hukumu itatolewa kesho.

ZeroDegree.
Hatima ya Ester Bulaya kujulikana kesho. Hatima ya Ester Bulaya kujulikana kesho. Reviewed by Zero Degree on 11/17/2016 08:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.