Loading...

Rais Magufuli atia saini sheria ya habari ya mwaka 2016.

RAIS John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli ametia saini sheria hiyo jana ikiwa ni siku 15 baada ya kupitishwa na Bunge la 11 la Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.

Aidha Rais amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.

"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa," alisema Rais Magufuli.

Zerodegree.
Rais Magufuli atia saini sheria ya habari ya mwaka 2016. Rais Magufuli atia saini sheria ya habari ya mwaka 2016. Reviewed by Zero Degree on 11/17/2016 04:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.