Ibrahimovic atoa ya moyoni mwake Man U.
Mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic anaamini klabu yake ya Manchester United ina ubavu wa kufikia mafanikio ya klabu aliyokuwa zamani, Paris Saint-Germain (PSG) kwenye soka England na Ulaya.
Hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Sweden alieleza kuwa hamu yake ya kujiunga na kocha Jose Mourinho ilirahisisha kazi yake ya kusajiliwa na klabu hiyo.
Mchezaji huyo alitua Old Trafford akiwa mchezaji huru msimu huu baada ya miaka minne ya mataji akiwa PSG na kueleza kuwa angehamishia mafanikio hayo Manchester United, alikoanza kwa karamu ya mabao.
United haijashinda taji la Ligi Kuu, EPL tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wao mwenye mafanikio makubwa, Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwisho wa msimu wa 2012-13 na msimu uliopita ilishinda Kombe la FA, ambalo ndilo la kipekee kwao.
Ibrahimovic, alieleza kuwa zipo changamoto lukuki za kuipa mafanikio makubwa United ili kuirejesha kileleni, akitaka kazi ngumu kwa wachezaji kujituma na ushirikiano wa bosi wake wa zamani, Jose Mourinho, aliyefanikisha uhamisho wake.
“Uwapo wa Mourinho kwangu ulikuwa wa maana katika kuifikiria United. Nilisaini kucheza kwa mwaka hapa, lakini jambo kubwa kwangu lilikuwa ni kuungana na Mourinho aliyenitaka nifanye uamuzi ambao ulikuswa rahisi,” alieleza Ibrahimovic akizungumza na Aftonbladet.
“Akinipigia simu sina tatizo naye, nilichotaka ni kuamua nini cha kufanya, nilipotambulishwa kama mchezaji wa United. Mengine si kwa sababu ya fedha.
“Nilichofuata hapa ni changamoto, kamwe sitasema sikutani nazo, zipo ni nyingi. Hiki ndicho nilichokuta, kuja hapa (United) na kukutana na watu, kuchezea moja ya klabu kubwa duniani, hilo halikuwa tatizo, nilitaka pia kujaribu soka kwenye Ligi ya England. Hiyo, ndiyo changamoto,” aliongeza
Msimu huu, United imekuwa na wakati mgumu, ingawa imeanza kupata mafanikio, ipo nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi tisa, lakini Ibrahimovic hashangazwi na matokeo hayo wala kiwango chao cha sasa.
“Nilisema tangu mwanzo sisi ni watu wadogo, hakuna nafasi ya kuwa mabingwa, tunaonekana hivyo kwa kila mmoja,” alisema.
Hadi sasa, Ibrahimovic ameifungia United mabao sita kwenye mechi 11 za EPL.

ZeroDegree.
Ibrahimovic atoa ya moyoni mwake Man U.
Reviewed by Zero Degree
on
11/26/2016 09:14:00 AM
Rating: