Ibrahimovic kuikosa Arsenal Novemba 19 baada ya kupata kadi ya njano ya 5 ya msimu huu.

Zlatan alipata kadi hiyo kunako dk ya 76 baada ya kumchezea vibaya Leroy Fer , na matokeo yake atakosa mechi dhidi ya washika bunduki wa London itakayopigwa Old Trafford mara baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Msweden huyo alipata kadi ya njano ya kwanza msimu huu kwenye mechi dhidi ya Man City Sept,10 na nyingine akipata walipocheza dhidi ya Stoke, Liverpool, Man City (EFL Cup) na ya tano dhidi ya Swansea.
ZeroDegree.
Ibrahimovic kuikosa Arsenal Novemba 19 baada ya kupata kadi ya njano ya 5 ya msimu huu.
Reviewed by Zero Degree
on
11/07/2016 04:10:00 PM
Rating:
