Loading...

George Lwandamina ajiuzulu kuifundisha klabu ya ZESCO.

Klabu ya Zesco ya Zambia leo imethibitisha kuwa Kocha wao Mkuu George Lwandamina amejiuzulu kuifundisha klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Kabu Katebe Chengo, imethibitisha kuwa Kocha msaidizi Tenant Chembo ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda.

Lwandamina amekuwa akihusishwa kusaini mkataba na mabingwa wa Tanzania Yanga, hali iliyopelekea kujiuzulu kwa Kocha Hans Van Pluijm kabla ya kubadili uamuzi wake na kuendelea na kazi.

Kocha huyo mwenye miaka 53 ameiwezesha Zesco kushinda ubingwa wa Zambia mara mbili, Kombe la Barclays, pamoja na kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

ZeroDegree.
George Lwandamina ajiuzulu kuifundisha klabu ya ZESCO. George Lwandamina ajiuzulu kuifundisha klabu ya ZESCO. Reviewed by Zero Degree on 11/07/2016 04:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.