Loading...

TB Joshua atabiri mshindi wa urais Marekani.

Muhubiri TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo dhidi ya mpinzani wake.
Muhubiri maarufu wa vipindi vya Televisheni nchini Nigeria TB Joshua amesema ametabiri " kwamba Hillary Clinton atamshinda Donald Trump" katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali tarehe 8 Novemba mwaka huu.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto nyingini - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi yake.

"boti ya rais mpya itakuwa imefungwa," aliongeza.

TB Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa "utabiri " wake ni wa uhakika.

Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
TB Joshua atabiri mshindi wa urais Marekani. TB Joshua atabiri mshindi wa urais Marekani. Reviewed by Zero Degree on 11/07/2016 04:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.