Loading...

Jecha uso kwa uso na wadau wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha.
TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inapanga kukutana na wadau wa uchaguzi kabla ya kuzichoma moto karatasi za wapiga kura zilizotumika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka jana na wa marudio uliyofanyika Machi 20, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa tume hiyo, Salum Kassim Ali, alisema utaratibu huo wa kukutana na wadau wa uchaguzi umeanza kufanyika ikiwamo vyama vya siasa.

“Baada ya kukutana na wadau wa uchaguzi karatasi za wapiga kura zilizotumika katika uchaguzi zitachomwa moto zikiwamo zilizotumika katika uchaguzi wa Oktoba, mwaka jana,” alisema Salum.

Alisema karatasi za wapiga kura ni nyaraka za serikali hivyo haziwezi kuchomwa moto bila ya kufuata taratibu ikiwamo kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kabla ya kuteketezwa.

Aidha, Salum alisema ZEC inaendelea kukamilisha ripoti ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na kwamba hatua kubwa imefikiwa kabla ya kukabidhiwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

“Tumefikia hatua kubwa ya kukamilisha ripoti ya uchaguzi, ndani ya mwezi huu tutakuwa tumekamilisha na kuikabidhi serikalini,” alisema.

Salum alisema ripoti hiyo itazingatia mambo mbalimbali yakiwamo mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa mwaka jana, pamoja na wa marudio uliyofanyika mwaka huu.

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ulilazimika kufanyika mara mbili baada ya uchaguzi wa kwanza wa Oktoba 25, mwaka jana matokeo kufutwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kwa madai ya kufanyika vitendo vya udanganyifu.

Uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu, huku Chama cha Wananchi (CUF) ambacho ndiyo chama kikuu cha upinzani Zanzibar kikisusia uchaguzi huo kikitaka uchaguzi wa awali ndiyo utambulike.

Source: Nipashe
ZeroDegree.
Jecha uso kwa uso na wadau wa uchaguzi.   Jecha uso kwa uso na wadau wa uchaguzi. Reviewed by Zero Degree on 11/04/2016 01:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.