Loading...

Kamanda Sirro pamoja na Suzane Kaganda kuchunguzwa na jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limesema litafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro na baadhi ya makanda wa mikoa ya kipolisi iliyoko katika kanda hiyo akiwemo kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzane Kaganda.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz katika makao makuu ya Polisi yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya CP Boaz kwa niaba ya jeshi la polisi imetolewa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni kuwatuhumu makamanda hao kuwa wanasita kuwachukulia hatua watumiaji na wauzaji wa kilevi cha shisha kwa madai kuwa huenda wakawa wamepokea rushwa kutoka kwa wanaojishughulisha na biashara hiyo, licha ya yeye ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika kanda hiyo kutoa maagizo wahusika kuchukuliwa hatua.

CP Boaz amesema kuwa “Kuhusu tuhuma ya rushwa hili suala lina taasisi zake zinazohusika, sisi tumepokea tuhuma hizo dhidi ya askari wetu kwa hiyo tunazichunguza kama ni kweli”

Credits: Dewij Blog
ZeroDegree.
Kamanda Sirro pamoja na Suzane Kaganda kuchunguzwa na jeshi la Polisi. Kamanda Sirro pamoja na Suzane Kaganda kuchunguzwa na jeshi la Polisi. Reviewed by Zero Degree on 11/18/2016 04:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.