Loading...

Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa nchini Afghanistan.

Kumeripotiwa shambulizi kubwa lililofanywa na wanamgambo kwenye kambi kubwa zaidi ya wanajeshi wa Marekani ya Bagram nchini Afghanistan.

Jeshi linaloongozwa na NATO, lilisema kuwa watu wanne waliuawa na hadi 14 kuejruhiwa wakati kifaa kimoja kililipuliwa.

Maafisa wanasema kwa huenda mlipuaji alikuwa ni mshambuliaji wa kujitoa mhanga, ambaye alidanganya kuwa mfanyakazi wakati wafanyakazi walikuwa wakiwasili katika kambi hiyo kwa shughuli za siku.

Kundi la Taliban linasema kuwa ndilo lilihusika. Hakuna taarifa zaidi kuhusu uraia wa wale waliouawa.

ZeroDegree.
Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa nchini Afghanistan. Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa nchini Afghanistan. Reviewed by Zero Degree on 11/12/2016 12:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.