Loading...

Kiungo machachali toka klabu ya Zesco atua Jangwani.

Kiungo wa Zesco United Justine Zulu tayari ametua nchini akitokea Zambia kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Yanga.

Kwa namna yoyote, hayo ni mapendekezo ya kocha George Lwandamina ambaye tayari ameanza majukumu ya kuifundisha Yanga ambapo jana Jumatatu Novemba 28 alisimamia mazoezi ya klabu hiyo kwa mara ya kwanza akiwa kocha mkuu mpya aliyechukua nafasi ya Hans van Pluijm.

Kwa muda mrefu Yanga imekuwa na wachezaji wachache wa eneo la kiungo wa katikati (Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Makapu na Mbuyu Twite) ukilinganisha na washindani wao wa ndani Simba na Azam FC ambao wanawachezaji wengi katika idara hiyo.

Justine Zulu anamiaka 27 amezaliwa 11 August 1989 Lusaka, Zulu amewahi kuvitumikaia vilabu vya National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United.

Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. October 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadae alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa.

Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012.


ZeroDegree.
Kiungo machachali toka klabu ya Zesco atua Jangwani. Kiungo machachali toka klabu ya Zesco atua Jangwani. Reviewed by Zero Degree on 11/29/2016 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.