Loading...

Sanchez anavyozidi kumkuna Arsene Wenger.

STRAIKA Alexis Sanchez anaonekna kuzidi kumkuna kocha wake, Arsene Wenger, baada ya Mfaransa huyo kusema kuwa amebaki ameduwaa kwa uwezo wake wa kubadili mchezo, baada ya kuiwezesha Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth, licha ya kuonekana kwa wengi kama amechoka.

Kwa sasa staa huyo raia wa Chile anaonekana kutakata tangu alipohamishiwa kwenye safu ya kiungo mshambuliaji, ambapo hadi sasa ameshafunga mabao saba katika mechi nane alizocheza katika mashindano yote, ikiwamo ya juzi dhidi ya Bournemouth.

Katika mchezo huo, uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates, vijana hao wa Kocha Eddie Howe walionekana kukaza, lakini kutokana na kiwango kizuri walichokionesha nyota wa Arsenal wakajikuta wakielemewa na kumfanya Sanchez apachike bao lake la pili katika muda wa nyongeza.

Kiwango hicho ndicho kinachomfanya Wenger kuendelea kubaki kinywa wazi na uwezo wa nyota huyo wa zamani wa Barcelona kwa vitu anavyovifanya uwanjani.

“Hata kama anaonekna ni mchovu, lakini bado yupo kwenye ubora na amekuwa akifanya vitu adimu anapokuwa na mpira,” alisema kocha huyo.

“Hali hiyo anakuwa nayo wakati mpira unapomfikia, mara zote huwa anatafuta gia nyingine ili aweze kuwa mtu hatari,”aliongeza kocha huyo.

Kwa sasa Sanchez anaripotiwa kumezewa mate na timu za Juventus na Manchester City, wakati akijiandaa kuingia miezi yake yake 18 ya mwisho kwenye mkataba wake na Wenger anafahamu Arsenal ni lazima ifanye kila iliwezalo ili kuhakikisha anabaki.


ZeroDegree.
Sanchez anavyozidi kumkuna Arsene Wenger. Sanchez anavyozidi kumkuna Arsene Wenger. Reviewed by Zero Degree on 11/29/2016 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.