Loading...

UEFA: Leicester City watoka kifua mbele dhidi ya Club Brugge kwa ushindi wa goli 2 - 1.

Leicester iliutawala vyema mchezo huo.
Leicester city wamepata ushindi maridhawa wakati wa muendelezo wa ligi ya mabigwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya club Brugge.


Leicester wanahitaji alama moja tu kutinga hatua ya mtoano.

Leicester hawajapoteza mchezo wowote ligi ya mabingwa Ulaya.
Mchezaji Shinji Okazaki alimaliza vyema kazi ya Christian Fuchs na kuandika goli la kwanza kwa kikosi hicho kinachonolewa na Muitaliano Claudio Ranieri.

Riyad Mahrez akaongeza goli la pili kwa penati murua ikiwa ni goli lake la nne ndani ya ligi ya mabigwa baada ya Marc Albrighton kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Leicester city hawashikiki katika ligi ya mabingwa Ulaya huku wakiwa wanaboronga EPL.

Dotmund wanakuwa timu ya nne kufunga magoli nane katika mchezo mmoja

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana:

  • Monaco 2-1 Tottenham
  • Borussia Dortmund 8-4 Legia Warsaw
  • Sporting 1- 2 Real Madrid
  • CSKA Moscow 1- 1 Bayer 04 Leverkusen
  • FC Copenhagen 0-0 FC Porto
  • Dinamo Zagreb 0-1 Olympique Lyonnais
  • Sevilla 1- 2 Juventus
ZeroDegree.
UEFA: Leicester City watoka kifua mbele dhidi ya Club Brugge kwa ushindi wa goli 2 - 1. UEFA: Leicester City watoka kifua mbele dhidi ya Club Brugge kwa ushindi wa goli 2 - 1. Reviewed by Zero Degree on 11/23/2016 10:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.