Loading...

Maamuzi yaliyotolewa na Shirikisho la soka la Uingereza [ FA ] baada ya kumkuta Jose Mourinho na hatia.

Hatimaye Chama cha Soka Uingereza (FA) kimetoa maamuzi ya kesi mbili ambazo zilikuwa zinamwandama kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kwa kukiuka sheria ambazo zimewekea katika Ligi Kuu nchi hiyo (EPL).

Kocha Mourinho alikuwa akishitakiwa kwa kosa la kuzungumza kuhusu mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mchezo wa Man United na Liverpool na kumtolea maneno mabaya mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo wa Man United na Burnley.

Katika kosa la kumtolea maneno mabaya mwamuzi Mark Clattenburg, Mourinho amefungiwa mchezo mmoja ambao utakuwa wa Swansea City utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii na atarejea katika mchezo wa Arsenal utakaopigwa Old Trafford, Novemba, 19.

Kuhusu kumzungumzia mwamuzi Anthony Taylor, Mourinho amepigwa faini ya Pauni 50,000 pamoja na kupewa onyo la kumtaka kuacha kuzungumza kuhusu waamuzi kabla ya mchezo.

ZeroDegree.
Maamuzi yaliyotolewa na Shirikisho la soka la Uingereza [ FA ] baada ya kumkuta Jose Mourinho na hatia. Maamuzi yaliyotolewa na Shirikisho la soka la Uingereza [ FA ] baada ya kumkuta Jose Mourinho na hatia. Reviewed by Zero Degree on 11/03/2016 09:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.