Loading...

Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa zilizochezwa jana Novemba 2.

Klabu bingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo ikiwa bado katika hatua za makundi.

Mchezo wa kusisimua zaidi ukiwa kati ya Legia Warsaw dhidi ya Real Madrid ambao ulikuwa wa piga nikupige.

Huku ikishuhudiwa Gareth Bale akifunga goli la kusisimua zaidi. Matokeo ya mwisho Legia Warsaw 3-3 Real Madrid.

Mchezo huo ulikuwa bila ya mashabiki wa Legia baada ya kufungiwa na Uefa.
Monaco ikiwa nyumbani imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya CSKA ya Moscow.

Tottenham Hotspur pia ikiwa nyumbani katika dimba la Wembley ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Tottenham walitumia uwanja wa Wembley badala ya White Hart Lane.
Leicester City ikiwa ugenini ililazimishwa sare tasa dhidi ya FC Copenhagen.

Matokeo ya michezo mingine.

  • Borussia Dortmund 1-0 Sporting
  • FC Copenhagen 0-0 Leicester city
  • FC Porto 1-0 Club Brugge
  • Juventus 1-1 Lyon
  • Sevilla 4-0 Dinamo Zagreb
ZeroDegree.
Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa zilizochezwa jana Novemba 2. Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa zilizochezwa jana Novemba 2. Reviewed by Zero Degree on 11/03/2016 09:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.