Loading...

Ndege za ATCL zaanza safari za Mwanza - Dar.

WAKAZI wa Jiji la Mwanza wanatarajia kupata zaidi fursa za kiuchumi baada ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuzindua rasmi safari zake jijini humo juzi.


Uzinduzi huo mbali na kuwanufaisha kiuchumi pia utafungua milango kwa watalii kutembelea vivutio vilivyopo katika mkoa huo, ikiwemo visiwa maarufu vya Saanane na Ukerewe.

Wakizungumzia uzinduzi wa safari hizo kwa kutumia ndege mpya ya shirika hilo aina ya Bombardier dash 8 - Q400, abiria walipongeza hatua ya serikali kulifufua shirika hilo na kuitaka isikubali kurudia makosa ya nyuma.

Mkazi wa Dar es Salaam, Charles Novat alisema, huduma za shirika hilo ni nzuri japo kuna maeneo yanayohitaji maboresho zaidi na kueleza kuwa ni fursa nzuri ya kukuza uchumi katika jiji hilo.

Kwa upande wake, Wakili wa kujitegemea wa kampuni ya Amitie Attorneys, Steven Makwega alipongeza ubora wa huduma za shirika hilo huku akishauri uwezekano wa kuangalia upya gharama za nauli ili kila Mtanzania aweze kumudu.

Alisema kwa kiwango cha nauli kilichopo si kila mmoja anaweza kumudu na pia wanatakiwa kuangalia vipindi kama vya mwisho wa mwaka ambavyo wanaweza wakapunguza gharama ili kutoa nafasi kwa watu wengi kujumuika na ndugu zao.

Akizungumza baada ya kufika jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuliho (Uchukuzi) alisema, kuhusu suala la gharama watajitahidi kuweka nauli ambazo kila mtanzania atamudu na kufurahia huduma za shirika hilo.

ZeroDegree.
Ndege za ATCL zaanza safari za Mwanza - Dar. Ndege za ATCL zaanza safari za Mwanza - Dar. Reviewed by Zero Degree on 11/03/2016 09:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.