Loading...

Msanii wa filamu nchini India aonekana amebeba nguruwe kwenye foleni ya ATM nje ya benki.

Watu wakiwa katika foleni nje ya benki.
Nyota wa filamu nchini India amezua hisia baada ya kupigwa picha akiwa amesimama katika foleni nje ya benki akiwa amebeba mwana wa nguruwe.

Ravi Babu amesema kuwa nguruwe huyo atashiriki katika filamu yake mpya kwa jina Adhigo ikimaanisha kutoka Telugo hadi ''there''.

Milolongo mirefu ya benki imekuwa kitu cha kawaida baada ya noti za rupee za 500 na 1000 kupigwa marufuku nchini humo katika vita dhidi ya ufisadi.

''Nilikuwa nikimpeleka ili kupigwa picha nilipogundua kwamba sina fedha za mafuta'',Babu aliambia BBC.

Ravi Babu akibeba mwana wa nguruwe.

''Nilisimama katika eneo la ATM lakini nikalazimika kumbeba mimi mwenyewe baada ya kupiga kelele wakati msaidizi wangu alipojaribu kumbeba.Lazima umbebe ikiwa mkono wako uko katika kifua chake na umuweka karibu nawe ili ajihisi vyema''.

Picha hiyo imesambazwa katika mitandao ya kijamii nchini India.

kumekuwepo na visa vya ghasia nchini India tangu marufuku hiyo ya noti itangazwe ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi wiki mbili zilizopita.

Watu wamekuwa wakipiga foleni kwa saa kadhaa nje ya benki pamoja na mashine za ATM ambazo huenda zikaishiwa na fedha.

Hatua hiyo imeathiri uchumi wa India.

ZeroDegree.
Msanii wa filamu nchini India aonekana amebeba nguruwe kwenye foleni ya ATM nje ya benki. Msanii wa filamu nchini India aonekana amebeba nguruwe kwenye foleni ya ATM nje ya benki. Reviewed by Zero Degree on 11/28/2016 10:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.