Loading...

Ofa ya Thomas Ulimwengu ni kufuru.

OFA ambayo straika wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, amewekewa mezani na mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Al Ahly ya Misri ni kufuru.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imepatikana na kuthibitishwa na wa staa huyo Jamal Kisongo, inasema kuwa Al Ahly wameweka mezani ofa ya mshahara wa Dola 400,000 (sawa na Sh milioni 860) kwa ajili ya straika huyo wa zamani wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kasongo alisema ofa hiyo inamaanisha kuwa kwa mwezi Ulimwengu atakuwa analipwa Dola 33,000 (sawa na Sh milioni 71.6) dau ambalo ni refu sana ikilinganishwa na wachezaji wengi wanaocheza ndani ya nchi.

Kisongo aliendelea kusema kuwa licha ya dau hilo kutamanisha, lakini wamelitolea nje kwa sababu ndoto zao ni kuhakikisha straika huyo mwenye miaka 23 anacheza nje ya bara la Afrika.

Alisema mbali na Al Ahly, Ulimwengu pia ana ofa kutoka Sudan, Afrika Kusini pamoja na nje bara la Afrika katika nchi za Urusi, Ubelgiji, Hispania, Qatar na China, ingawa hakutaja klabu gani zinamuwania.

Kisongo ambaye pia ni Meneja wa Mbwana Samatta, aliongeza kusema kuwa kuna timu moja ya Ligi Kuu Ubelgiji na nyingine Daraja la Kwanza England pia zinamhitaji kwenda kufanya majaribio, lakini wamekataa kwa sababu Ulimwengi si mchezaji wa majaribio.

Meneja huyo alisema kinachosababisha Ulimwengu kuchelewa kujiunga na timu hizo ni majeraha ya goti aliyoyapata katika moja ya mechi za Kombe la Shirikisho Afrika wakati akiwa TP Mazembe kabla ya timu hiyo kuchukua ubingwa mwaka huu.

“Ulimwengu kwa sasa amepona na ameanza mazoezi ya utimamu wa mwili, lakini amepata mwaliko wa kwenda kufanya mazoezi katika klabu ya Mamelody Sundown inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini,” alisema Kisongo.

Ulimwengu alitokea katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu Copa Coca cola na baadaye kulelewa katika Kituo cha Tanzania Soccer Academy (TSA) kilichokuwa chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kabla ya kwenda Sweden na kujiunga na TP Mazembe.

Credits: Bingwa
ZeroDegree.
Ofa ya Thomas Ulimwengu ni kufuru. Ofa ya Thomas Ulimwengu ni kufuru. Reviewed by Zero Degree on 11/28/2016 10:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.