Rais Magufuli amepiga marufuku majeshi kuingia ubia na watu binafsi.
Rais John Magufuli Rais amepiga marufuku majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi, kupangisha au kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka sehemu zote za majeshi zibaki katika jeshi husika.
Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alisema hayo jana baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam. Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu haikufafanua zaidi kuhusu suala hilo.
Hatua hiyo inatarajiwa kuzua mshikemshike katika baadhi ya maeneo ya jeshi ambayo baadhi ya raia ama wamepangisha au kujenga vibanda kwa ajili ya biashara.
Mbali ya marufuku hiyo, pia Rais Magufuli amepiga marufuku watu binafsi kuuza wa sare za majeshi nchini na kutaka wale wote wanaofanya hivyo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza kuwa Rais ametoa agizo hilo baada kupata maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini.
Alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi.
‘’Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu,” alisema Rais Magufuli.

Mbali na maagizo hayo, Rais Magufuli ametoa Sh10 bilioni kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya za makazi ya askari katika Gereza la Ukonga.
Alisema hayo baada ya kusikiliza malalamiko ya askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji wao wa kazi.
Rais Magufuli amewahakikishia maofisa na askari wa Magereza kuwa Serikali itaendelea kuboresha masilahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini.
Pia, amelitaka jeshi hilo kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi na kuzalisha tofauti na mfumo wa sasa ambao baadhi ya wafungwa wanatumia rasilimali za Serikali bila kuzifanyia.

ZeroDegree.
Rais Magufuli amepiga marufuku majeshi kuingia ubia na watu binafsi.
Reviewed by Zero Degree
on
11/30/2016 12:56:00 PM
Rating: