Loading...

Sakata la usajili wa Hassan Kesi bado ni utata.

Shirikisho la soka nchini TFF bado linaendelea kulipiga danadana suala la beki wa pembeni Hassan Ramadhan ‘Kessy’ ambaye ameshitakiwa na uongozi wa klabu ya Simba kwa kosa la kuvunja mkataba na kujiunga na Young Africans mwishoni mwa mwa msimu uliopita.

TFF walitarajiwa kutoa maamuzi ya kesi ya mchezaji huyo kupitia kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji, lakini ilishindwa kufanya hivyo na kuwataka viongozi wa klabu hizo kongwe kuketi pembeni na kuzungumza ili wamalizane.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa shirikisho la soka nchini Alfred Lucas amesema mpaka sasa viongozi wa pande hizo mbili wameshindwa kupata suluhu, kutokana na sababu ambazo zilikua nje ya uwezo wao.

“Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ilikaa weekend iliyopita na pande zote zilikuwepo (Yanga na Simba), tukawaomba kutoa ripozi zao walipofikia kwenye suala la usuluhishi, Simba walikuwa tayari kutoa taarifa lakini Yanga walikwama.”

“Yanga wakatoa udhuru kwamba, wakili wao (Alex Mgongolwa) ambaye angeweza kulizungumzia suala hilo amepata matatizo ya kifamilia na alisafiri kwenda Iringa kushiriki msiba.”

“Kwakuwa hakuwepo wakili wakili wa Yanga, msuluhishi wa suala hilo mzee Said El Maamry alisema ili kutenda haki, ni vyema mwanasheria wa Yanga asubiriwe afike.”

“Kikao hicho kimeahirishwa hadi November 3, 2016 saa 11 jioni kwenye ukumbi wa TFF, na kama itashindikana kukubaliana kwa namna yeyote ile suala hilo litarudi kwenye kamati kwa maamuzi ya mwisho.”

ZeroDegree.
Sakata la usajili wa Hassan Kesi bado ni utata.  Sakata la usajili wa Hassan Kesi bado ni utata. Reviewed by Zero Degree on 11/02/2016 12:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.