Loading...

Samatta kutua Man U.

HUENDA ndoto za Mtanzania, Mbwana Samatta, kuchezea timu ya Manchester United ikatimia baada ya msaka vipaji mkuu (skauti) wa klabu ya KRC Genk anayochezea straika huyo kulamba dili kwa Mashetani hao Wekundu.

Roland Janssen ambaye alikuwa skauti wa kikosi hicho cha Genk kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, amepata dili la kuajiriwa Man United na huenda huo ukawa mwanzo wa Samatta kupiga hatua moja mbele.

Kazi kubwa ambayo skauti huyo amepewa na Manchester United ni kutafuta wachezaji wanaocheza ligi ya Ubelgiji wenye uwezo mkubwa na kuwaunganisha na Mashetani hao wekundu.

Kupata dili kwa skauti huyo kunaashiria kuwa njia sasa ni njeupe kwa Samatta kupata nafasi ya kwenda kucheza soka nchini England kama ataongeza bidii katika kikosi chake cha Genk.

Skauti huyo alikuwa chanzo cha Samatta kutoka TP Mazembe na kujiunga na Genk na sasa anaweza pia kuwa daraja la kumtoa Genk na kujiunga na Man United ya Jose Mourinho.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya Congo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiibuka kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani huku kikosi chake hicho kikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

ZeroDegree.
Samatta kutua Man U. Samatta kutua Man U. Reviewed by Zero Degree on 11/09/2016 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.