Loading...

Shirikisho la Soka Tanzania [ TFF ] kupangua ratiba ya ligi kuu Tanzania bara.

RATIBA ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara mzunguko wa pili huenda ikapanguliwa kupisha mashindano ya maalumu ya Krismasi yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 15 hadi Januari mosi 2017.

Taarifa za ndani ambazo gazeti hili imezipata kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo, zinasema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu nane kutoka nchi za Afrika Mashariki na Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

"Tumeshafanya vikao vinne hivi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano haya pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na tumefikia muafaka na yanatarajiwa kuanza Desemba 15," kilisema chanzo hicho.

Mashindano haya yamebuniwa baada ya kushindikana kufanyika mashindano ya Kagame ambayo hushirikisha timu kutoka mashirikisho wanachama wa Baraza la Soka la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Timu zinazotarajiwa kushiriki ni Simba na Yanga za Tanzania, Vital'O ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya, KCCA ya Uganda, Rayon Sporting ya Rwanda. Timu nyingine ni Ferreviaro de Beira ya Msumbiji na Athletico.

ZeroDegree.
Shirikisho la Soka Tanzania [ TFF ] kupangua ratiba ya ligi kuu Tanzania bara. Shirikisho la Soka Tanzania [ TFF ] kupangua ratiba ya ligi kuu Tanzania bara. Reviewed by Zero Degree on 11/26/2016 10:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.