Loading...

Hizi ndizo ajali za Ndege zilizosababisha vifo vya wachezaji wengi zaidi Duniani.

Story ya kuanguka kwa ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya Chapecoense ya Brazil imechukua headlines kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii dunia nzima, huku likiwa tukio ambalo limeacha majonzi kwenye familia ya soka ulimwenguni.


Ndege hiyo ilianguka kwenye mji wa Medellin baada ya kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme. Klabu hiyo ilikuwa inakwenda kucheza mchezo wa raundi ya kwanza ya fainali ya kombe la Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.

Kulikuwa na watu 81 ndani ya ndege hiyo, 72 wakiwa ni abiria (wachezaji, benchi la ufundi na viongozi) huku 9 wakiwa ni wafanyakazi wa ndege hiyo. Kati ya watu 81 waliokuwemo katika ndege hiyo ni watu 5 ndio wametoka salama na 76 wameripotiwa kupoteza maisha.






Ajali nyingine za ndege ambazo zinakumbukwa kwa kugharimu maisha ya wachezaji wengi kwa wamati mmoja ni pamoja na:

The grande Torino (1949)


The Grande Torino ilikuwa kikosi cha kihistoria cha timu ya Torino Football Club kilichokuwa ni mabingwa mara tano wa Italy ambacho wachezaji wake walikuwa ni uti wa mgongo wa timu ya taifa ya Italia.

Walikufa kwenye ajali ya ndege May 4, 1949 ajali hiyo ni maarufu kwa jina la Superga air disaster.

Torino tunayoiona leo, enzi hizo ilikuwa na kikosi bora kabisa kikosi ambacho kinatoka nchini Ureno kucheza mechi dhidi ya Benfica, watu wote (31) waliokuwemo kwenye ndege wakapoteza maisha wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi pamoja na waandishi wa habari.

Munich Disaster Manchester United (1958)


Mwaka 1968 kikosi cha Manchester United kilipoteza baadhi ya wachezaji kutokana na ajali ya ndege iliyotokea wakati ndege hiyo ikitaka kuruka huko mjini kwenye uwanja wa ndege wa Munich-Riem, Ujerumani Magharibi.

Kikosi cha Man United wakati huo kilikuwa maarufu kwa jina la “Busby Babes” kilishuhudia watu 20 kati ya 44 wakifariki papo hapoi na majeruhi wakapelekwa hospitali lakini wengine watatu wakafarika na kufikia idadi ya watu 23 waliopoteza maisha huku wengine 21 wakinusurika kifo.

Miongoni mwa watu walionusurika ni pamoja na Bobby Charlton pamoja na kocha wao Matt Busby.

Zambia national football team air disaster (1993)


Ilikuwa ni jioni ya April 27 1993 ndege iliyokuwa imebeba abiria ambao kwa asilimia kubwa walikuwa ni wachezaji wa Zambia iliangua mita 500 kabla kutoka pwani ya mji wa Libreville, Gabon.

Wachezaji hao walikuwa wakielekea Dakar, Senegal kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kucheza kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Senegal.

Ajali hiyo ilipoteza maisha ya wachezaji wote 18 wa kikosi cha Zambia, benchi la ufundi, wafanyakazi wa ndege hiyo pamoja na watu wengine.

ZeroDegree.
Hizi ndizo ajali za Ndege zilizosababisha vifo vya wachezaji wengi zaidi Duniani. Hizi ndizo ajali za Ndege zilizosababisha vifo vya wachezaji wengi zaidi Duniani. Reviewed by Zero Degree on 11/30/2016 11:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.