Loading...

Wachimbaji wadogo watatu wa madini wapoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo.

Wanawake watatu wachimbaji wadogo wa madini wa eno la Zambi lililopo katika kitongoji na kijiji cha Matongo wilaya ya Iramba mkoani Singida, wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo wakiwa kazini wakichimba madini aina ya dhahabu.


Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Mayala Towo,aliwataja wanawake hao waliofariki dunia kuwa ni Anna Martine (56),Paulina Msingi (45) na Magreth Samwel (45),wote wakazi wa kijiji cha Mgongo.

Aidha,Towo alitaja majeruhi katika tukio hilo kuwa ni Amri Hamisi (34) na Sambo Msengi (16) wakazi wa kijiji cha Mgongo na wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

“Majeruhi wote wamelazwa katika kituo cha afya cha kijiji cha Mgongo na hali zao zinaendelea vizuri.Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi,” alisema.

Kaimu kamanda huyo,alisema tukio hilo limetokea oktoba mbili mwaka huu majira ya saa 7.40 mchana wakati wachimbaji hao wadogo wakiwa kwenye harakati za kuchimba dhahabu.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni wachimbaji hao kushindwa kuchukua tahadhari wakati wakifanya shughuli zao za uchimbaji.

Kaimu kamanda Towo,ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji kuchukua tahadhari wakiwa wanafanya shughuli za uchimbaji na wazazi/walezi wasiruhusu watoto wao walio chini ya umri wa miaka 18,kujishughulisha na kazi za uchimbaji madini.

ZeroDegree.
Wachimbaji wadogo watatu wa madini wapoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo. Wachimbaji wadogo watatu wa madini wapoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo. Reviewed by Zero Degree on 11/04/2016 03:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.