Loading...

Wakuu wa mikoa 7 hatarini kutumbuliwa.

Wakuu wa mikoa saba wamekalia kuti kavu kutokana na kushindwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati katika mikoa yao.

Akizungumza jana akipokea madawati 3,500 yenye thamani ya Sh300 milioni kutoka benki ya NMB, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene alisema mikoa ya wakuu hao saba inayoongoza kwa upungufu wa madawati ni Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma.

Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli.

ZeroDegree.
Wakuu wa mikoa 7 hatarini kutumbuliwa. Wakuu wa mikoa 7 hatarini kutumbuliwa. Reviewed by Zero Degree on 11/18/2016 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.