Loading...

Wanafunzi watatu wafa maji wakiogelea katika ziwa Tanganyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui.
WANAFUNZI watatu wamefariki dunia wakati wanaogelea katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Tukio hilo lilitokea jana saa 12:00 jioni eneo la Lutare ndani ya Ziwa Tanganyika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, alithibitisha vifo vya wanafunzi hao.

Kamanda Mtui alisema wanafunzi hao walipatwa na mkasa huo baada ya kupita katika ziwa hilo wakati wakitoka shuleni kwa lengo la kuogelea.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni Omari Ramadhani (11), mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kipampa, mkazi wa Buzebazeba, Haimani Kalenga (9), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Livingstone, mkazi wa Buzebazeba na Hussein Moshi (18), aliyekuwa akisoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Lusimbi mkazi wa majengo Ujiji.

Kamanda Mtui alisema miili ya wanafunzi hao ilipatikana ndani ya Ziwa Tanganyika na kuchukuliwa na kwenda kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni.

Aliongeza kuwa miili hiyo imehifadhiwa hospitalini hapo ikisubiriwa kuchukuliwa na ndugu zao ili taratibu za maziko ziendelee. Kamanda Mtui aliwataka wazazi na walezi kuzuia watoto wao kuogelea katika Ziwa Tanganyika, mabwawa na mito hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kuepukana na vifo vitokanavyo na maji.

ZeroDegree.
Wanafunzi watatu wafa maji wakiogelea katika ziwa Tanganyika.   Wanafunzi watatu wafa maji wakiogelea katika ziwa Tanganyika. Reviewed by Zero Degree on 11/10/2016 09:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.