Loading...

Wazazi wa wanafunzi watoro shuleni kufikishwa kwenye mikono ya sheria.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema wataanza kukamata wazazi wa watoto watoro na kufikishwa kwenye mikono ya sheria, akisisitiza mkoa hauwezi kupata maendeleo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaokatisha masomo huku idadi kubwa ikiwa ni wasichana.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Fufu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Alisema wazazi na walezi wana wajibu wa kuongeza bidii na kuhakikisha watoto wanaoshiriki vyema masomo yao.

“Wanaoanza darasa la kwanza sio wanaomaliza darasa la saba, lazima tuchukue hatua za makusudi kwani hatuwezi kupata madaktari, walimu na viongozi kama kukiwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito,” alisema.

Alisema wazazi na walezi wana wajibu wa kuwawezesha watoto wao kumudu maisha ya baadaye.

“Nitarudi tena kijiji hiki ili kuona changamoto ambayo imekuwa ikifanya wanafunzi wengi kukatisha masomo yao kuna utoro, kupata mimba,” alisema.

Alisema wazazi watafikishwa kwenye mikono ya sheria, kwani anataka Dodoma iendelee kuchangia uchumi wa taifa kama ilivyokuwa zamani, kwani Dodoma ina wajibu huo.

Pia Rugimbana amepiga marufuku wananchi kutumia chakula kwa ajili ya kupikia pombe.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino, Mussa Kawea alisema wataendelea kuhimiza wananchi kupanda miti ili kuboresha mazingira.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athumani Masasi alisema hivi karibuni atafanya ziara kwa baadhi ya vijiji wilayani humo kwa lengo la kusikiliza changamoto za wananchi na kuona namna ya kuzitatua.

ZeroDegree.
Wazazi wa wanafunzi watoro shuleni kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Wazazi wa wanafunzi watoro shuleni kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Reviewed by Zero Degree on 11/07/2016 09:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.