Loading...

Yanga yampotezea straika wao.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Anthony Matheo amemaliza mkataba na timu hiyo lakini bado yupo njia panda kwani uongozi wake umemchunia pasi na kumpa ukweli juu ya hatma yake wakati ligi ikienda mapumziko.

Matheo alisajiliwa Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea KMKM baada ya kung’ara kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Dar es Salaam miaka mitatu iliyopita huku Simba nao walikuwa wakiiwania saini yake.

Nyota huyo alisajiliwa Yanga kwa donge nono kuliko ofa ya Sh 7milioni aliyotakiwa kupewa na Simba, lakini anasema hadi sasa hajui hatma yake Jangwani kutokana na viongozi wa Yanga kuwa kimya.

“Mkataba wangu unamalizika mwezi huu kwa maana hiyo mzunguko wa pili utakapoanza utakuwa umekwisha, bado sijazungumza na Yanga na wala sijaambiwa lolote pengine ni kubanwa na ligi, ngoja tusubiri tuone,” alisema.

Akizungumza mzunguko huo kwa ujumla ambao Yanga wamemaliza wakiwa nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 33 huku Simba wakiongoza kwa pointi 35, Matheo alisema: “Nilikuwa sipati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi changu, mara kadhaa nilianzia benchi. Ila wenzangu walipambana kupata matokeo mazuri kwani hii ligi ni ngumu, nasi hatukupata muda kujiandaa.

“Mengi yamesemwa kuwa tunabebwa, mara tunafunga mabao ya mkono, ila tunachoangalia ni kile mwamuzi anachoamua na kupata pointi tatu pekee, hayo mengine ni maneno tu,” alisema Matheo.

Credits: Mwanaspoti
ZeroDegree.
Yanga yampotezea straika wao. Yanga yampotezea straika wao. Reviewed by Zero Degree on 11/12/2016 12:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.