Loading...

Ujerumani yaidhalilisha San Marino kwa kipigo cha goli 8 kwa sifuri, ..Gnabry atoka na hat-trick yake ya kwanza.

Kiungo wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry amefunga hat-trick yake ya kwanza wakati Ujerumani ikiifedhehesha timu ya taifa ya San Marino kwa kipigo cha magoli 8-0 wakati wa mchezo uliokuwa wa upande mmoja kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia.

Gnabry, ambaye kwa sasa anakipiga Werder Bremen, alifungua account yake dakika ya 10 na kufunga magoli mengine mawili kipindi cha pili na kuwa mchezaji wa kwanza Ujerumani kufunga magoli matatu kwenye mechi yake ya kwanza tangu Dieter Muller alipofanya hivyo mwaka 1976.

Magoli mengine yalifungwa na Sami Khedira, Jonas Hector (2) pamoja na Kevin Volland huku Mattia Stefanelli akijifunga kukamilisha ushindi wa magoli 8 kwa Ujerumani.

Ujerumani inaongoza Kundi C ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi nne tofauti ya pointi tano na timu zinazofata katika nafasi ya pili na ya tatu.

Gnabry, 21, alijiunga na Bremen kwa dau ambalo halikuwekwa wazi mwezi August baada ya kumaliza kama mfungaji bora kwenye michuano ya Olympic wakati Ujerumani ilipopoteza mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji Brazil.

“Sikufikiria kama nitafunga magoli matatu kwenye mchezo wangu wa kwanza,” anasema Gnabry, ambaye alijiunga na Arsenal akitokea Stuttgart mwaka 2001 na kufanikiwa kucheza mechi 18 na kufunga bao 1 akiwa na The Gunners.

ZeroDegree.
Ujerumani yaidhalilisha San Marino kwa kipigo cha goli 8 kwa sifuri, ..Gnabry atoka na hat-trick yake ya kwanza. Ujerumani yaidhalilisha San Marino kwa kipigo cha goli 8 kwa sifuri, ..Gnabry atoka na hat-trick yake ya kwanza. Reviewed by Zero Degree on 11/12/2016 12:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.