Loading...

Lyon watibua hesabu za Mgosi.

SIMBA imetibuliwa rekodi yake ya kutofungwa katika ligi ya msimu huu na timu iliyotibua rekodi hiyo ni African Lyon, kitu ambacho kimemtibulia straika wa zamani wa timu ambaye ni meneja wa timu kwa sasa, Mussa Hassan Mgosi.

Mgosi alinukuliwa hivi karibuni akisema anahamu ya kuona rekodi waliyoiweka msimu wa 2009-2010 kwa Simba kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo na huku ikitoa Mfungaji Bora ikijirudia msimu huu, lakini mambo yametibuka.

Simba juzi Jumapili ilifungwa na Lyon bao 1-0 kabla ya keshokutwa kukamilisha mechi yake ya 15 kwa kuvaana na Prisons ugenini jijini Mbeya.

Mgosi aliliambia Mwanaspoti kuwa kufungwa na Lyon kumewatibulia rekodi, lakini hakujawakatisha tamaa katika mbio zao za kubeba ubingwa kwani mechi zilizosalia bado ni nyingi.

“Makocha wameona makosa yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo iliyotufanya tupoteze pointi tatu, watayafanyia kazi ili mechi nyingine yasijirudie, tuwape moyo wachezaji ili kutimiza yale yote yaliyokusudiwa,” alisema na kuongeza;

“Kila mtu anafahamu kwenye mechi kuna matokeo ya aina tatu, kushinda, kufungwa na kutoka sare, Lyon walipata nafasi wakaitumia hata sisi tulipata ila tulishindwa kutumia.”

ZeroDegree.
Lyon watibua hesabu za Mgosi. Lyon watibua hesabu za Mgosi. Reviewed by Zero Degree on 11/12/2016 12:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.