Loading...

Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila aikimbia NCCR na kuhamia CHADEMA.

David Z. Kafulila
Aliyekuwa Katibu mwenezi wa NCCR – MAGEUZI David Z. Kafulila ametoa waraka wa wazi akitaarifu kuwa amejiengua na uanachama na nafasi aliyokuwa nayo katika chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Pamoja na mambo mengine, katika waraka huo Kafulila ameushukuru uongozi wa NCCR- MAGEUZI kwa muda wote aliokuwa nao. Pia akaeleza uamuzi wake wa kujivua nafasi yake ya uongozi na nia yake ya kufuata mabadiliko licha ya ukandamizwaji unaofanywa na vyombo vya kusimamia haki.

Kafulila ameeleza maoni yake ya kuunganisha nguvu na kuwa na chama kimoja cha upinzani chenye mikakati dhabiti ya kuleta mabadiliko na chama hicho si kingine bali ni Chadema.

ZeroDegree.
Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila aikimbia NCCR na kuhamia CHADEMA. Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila aikimbia NCCR na kuhamia CHADEMA. Reviewed by Zero Degree on 12/17/2016 09:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.