Aliyempeleka Mbwana Samatta KRC Genk atimuliwa.
MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amesikitishwa na kitendo cha klabu yake KRC Genk ya Ubelgiji kumfukuza kocha Peter Maes.
Genk jana ilitangaza kumtupia virago kocha huyo Mbelgiji baada ya kupata matokeo mabaya hivi karibuni na nafasi yake itashikwa na aliyekuwa msaidizi wake Rudi Cossey kwa muda.
Akizungumza kwa njia ya mtandao jana, Samatta aliyesajiliwa na Genk akitokea TP Mazembe ya Congo DR alisema taarifa hizo zimemsikitisha hasa kwa vile ndiye kocha aliyeuona uwezo wake na kumsajili.
"Si taarifa nzuri sana kwangu kwa sababu Maes aliniamini kwa muda mfupi na kunipa nafasi sasa anapoondoka inakuwa ngumu kidogo kuanza na kocha mwingine,” alisema.
Hata hivyo, Samatta alisema siri pekee ya kuendelea kuwavutia makocha ni kujituma zaidi na hilo ndilo analolifanya siku zote. Aidha, Samatta alimzungumzia kocha Maes kwamba alikuwa rafiki wa kila mchezaji na hakuwa na ufundishaji mgumu.
“Alifundisha kiasi ambacho mchezaji hakupata tabu kumuelewa,” alisema.
Chini ya Maes, Samatta amecheza mechi 35 Genk,18 msimu uliopita na 17 msimu huu huku akianza michezo 10 msimu uliopita na saba msimu huu.
Maes alijiunga na Genk msimu wa 2015-2016 kutoka KSC Lokeren na ameiongoza timu hiyo katika mechi 81.

ZeroDegree.
Aliyempeleka Mbwana Samatta KRC Genk atimuliwa.
Reviewed by Zero Degree
on
12/27/2016 01:42:00 PM
Rating: