Loading...

Arsenal wakubali kichapo cha pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza [EPL].

Beki wa Arsenal Hector Bellerin akikabilina na winga wa Manchester City Raheem Sterling.
Matajiri wa jiji la Manchester, Man City wakicheza katika dimba lao Etihad wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal.

Arsenal ndio walianza kupata goli katika dakika ya 5 ya mchezo kupita kwa Theo Walcott.

Wachezaji wa Arsenal wakishanglia goli la Theo Walcott.
Man City walisawazisha goli hilo katika pindi cha pili dakika ya 47 bao likiwekwa kambani na Leroy Sane.

Bao la ushindi la vijana wa Pep Guardiola lifungwa na winga Raheem Sterling katika dakika ya 71 ya mchezo.

Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Arsenal baada ya katikati ya wiki kupigwa 2-1 na Everton

Katika michezo mingine Tottenham iliichapa Burnley 2-1 na Southampton walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth.

Jumatatu Usiku kutapigwa dabi ya Merseyside. Ambapo Everton wataalika Liverpool katika dimba la Goodison Park.

ZeroDegree.
Arsenal wakubali kichapo cha pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza [EPL]. Arsenal wakubali kichapo cha pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza [EPL]. Reviewed by Zero Degree on 12/19/2016 05:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.