Loading...

Rais Kabila kumaliza muhula wake madarakani leo.

Muhula wa mwisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, unamalizika leo huku kukiwa hakuna dalili ya uchaguzi wa mrithi wake na upinzani ukisema hiyo ni hatua ya kubaki madaraka na kukiuka katiba.

Uchaguzi umeahirishwa hadi Aprili 2018 kwa madai ya maandalizi kutokamilika na matatizo ya kifedha huku pia Rais Kabila akifikia makubaliano na baadhi ya viongozi wa upinzani, makubaliano ambayo yanamaanisha yeye kuendelea kubaki madarakani.

Mahakama ya katiba imesema Kabila anaweza kubakia madarakani lakini kambi kuu ya upinzani imekataa makubaliano hayo ikisema ni njama za kuvuruga demokrasia.

Mazungumzo ya hivi karibuni yaliyoratibiwa na Kanisa Katoliki yalishindwa kufikia muafaka. Serikali imepiga marufuku maandamano mjini Kinshasa ambako ni ngome ya upinzani na kuongeza hofu na ukandamizaji mkubwa katika taifa hilo lililokumbwa na vita na kukosekana kwa utulivu.

ZeroDegree.
Rais Kabila kumaliza muhula wake madarakani leo. Rais Kabila kumaliza muhula wake madarakani leo. Reviewed by Zero Degree on 12/19/2016 05:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.