Loading...

DRC Congo kufunga Mitandao ya kijamii jumapili.

Kampuni za mitandao katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeamrishwa kufunga mitandao ya kijamii kwanzia Jumapili hii. Hii ni kwa mujibu wa shirika la habari AFP.

Mmoja wa maafisa wa kampuni ya mtandao amewambia AFP kwamba wamepokea amri hiyo kutoka kwa serikali kubana mtandao wote. Muhula wa Rais Joseph Kabila chini ya katiba unatarajiwa kumalizika Jumatatu ya wiki ijayo.

Wanaharakati wameanzisha kampeini kwenye Twitter #ByeByeKabila, kama njiya ya kumshinikiza kiongozi huyo kuachia ngazi. Chini ya katiba ya DRC Rais Kabila alistahili kumaliza muhula wake Decemba mwaka huu na kufanyike uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo tume ya uchaguzi ilisema haikuwa tayari kuanda uchaguzi. Mazungumzo ya kitaifa ambayo yalisusiwa na vyama vikuu vya upinzani yalipendekeza uchaguzi kuahirishwa hadi mwaka 2018, ambapo Kabila ataongoza kipindi cha mpito.

Licha ya kwamba mahakama ya kuu imeridhia makubaliano hayo, hata hivyo wapinzani wamesema lazima Kabila aondoke madarakani kwanza na kuundwe utawala wa mpito bila yeye kuongoza.

Rais huyo ameahidi kwamba hatagombea mwaka 2018, lakini wapinzani wamepinga hilo. Kumekua na maandamano yaliokumbwa na ghasia na vifo kushinikiza Joseph Kabila kuheshimu katiba ya nchi na kustaafu. Katiba haimkubalii kuwania Urais tena baada ya kumaliza mihula miwili.

ZeroDegree.
DRC Congo kufunga Mitandao ya kijamii jumapili. DRC Congo kufunga Mitandao ya kijamii jumapili. Reviewed by Zero Degree on 12/15/2016 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.