Ummy Mwalimu atoa matumaini kwa wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa mashuleni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema atahakikisha kwa dhamana aliyopewa anawashawishi wenzie waliopo serikalini ili wanafunzi wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na masomo.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF).
“Msichana akielimika utamlinda na mimba za utotoni, ndoa za utotoni, maambukizi ya VVU na Ukimwi lakini pia hatakubali kufanyia vitendo vya ukatili. Lwahiyo bado sisi ambao tumepewa dhamana ya kusimamia maendeleo ya watoto hasa watoto wa kike tutaendelea kuwashawishi wenzetu serikalini tuhakikishe kuwa watoto wa kike wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na masomo,” alisema Mwalimu.

ZeroDegree.
Ummy Mwalimu atoa matumaini kwa wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa mashuleni.
Reviewed by Zero Degree
on
12/15/2016 06:54:00 PM
Rating: