Arsene Wenger adai kwamba magoli waliyofungwa na Manchester City hayakua halali.
KWA kile unachoweza kusema kuwa anadai Man City walibebwa, kocha Arsene Wenger, amedai kuwa mabao waliyofungwa Arsenal juzi kwenye Uwanja wa Etihad, yote yalikuwa ni ya kuotea.
Juzi washika mtutu hao kutoka Kaskazini mwa Jiji la London, walichezea kichapo cha 2-1 yaliyowekwa kimiani na mastaa, Leroy Sane na Raheem Sterling kipindi cha pili, baada ya Theo Walcott kuipatia Arsenal bao la mapema kipindi cha kwanza.
Akizungumza na Kituo cha Sky Sport, Wenger alisema hawakuwa na nguvu kipindi cha pili kama walivyokuwa cha kwanza.
“Nadhani hatukuwa na nguvu kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza tulikuwa hatari muda wote na wenye kasi, lakini pamoja na yote mwamuzi hakuwa upande wetu,” alisema Mfaransa huyo.
“Mabao yote mawili yalikuwa ya kuotea na katika mechi ya namna ile, nadhani ilitosha kwa upande wetu. Tumekutana na maamuzi mabaya msimu wote na hasa leo (juzi) nimeyaangalia magoli yote, waliotea,” aliongeza Wenger.
“Goli la pili wamezidi kwa yadi tano. Na la kwanza hali kadhalika. Lakini nini naweza kufanya? Inabidi tukubali matokeo. Tunahitaji kujitathmini wenyewe na kujua ni kwanini tumepoteza mchezo,” aliongeza tena Mfaransa huyo.
Matokeo hayo yanamaanisha Arsenal wanashuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, pointi tisa nyuma ya vinara Chelsea.

ZeroDegree.
Arsene Wenger adai kwamba magoli waliyofungwa na Manchester City hayakua halali.
Reviewed by Zero Degree
on
12/20/2016 11:49:00 AM
Rating: