Loading...

Auawa kwa kuchomwa kisu akigombea soda.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.
MKAZI wa Kwamromboo jijini Arusha, Novatus Tadei, ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto katika ugomvi wa kugombea soda.

Tukio hilo la mauaji ya kijana huyo mwenye miaka 26 limetokea juzi kwenye shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo, tukio hilo lilitokea saa 2:00 usiku katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi eneo la Kwamromboo na polisi wanamshikilia Hamis Amani (17) mkazi wa Olasiti kuhusu tukio hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa Tadei pamoja na mtuhumiwa wanafanya kazi pamoja ya upishi kwenye kampuni inayojulikana kwa jina la ZZ Catering inayomilikiwa na Bashiri Ally, mkazi wa Kwamromboo.

Kamanda Mkumbo alisema siku ya tukio, Tadei pamoja na wafanyakazi wengine akiwemo mtuhumiwa baada ya kumaliza kazi walipanda gari aina ya Toyota Hiace lenye namba T375 CHH kwa lengo la kurejea nyumbani.

Alisema wakiwa ndani ya gari hilo, mtuhumiwa Hamis Amani aligundua kuwa soda aliyokuwa ameiweka ndani ya mfuko wake haipo na kuanza kuhisi Tadei ndiye aliyechukua jambo lililozua ugomvi baina yao na kuanza kutukanana.

Alisema Tadei alimkwida na mtuhumiwa kuchukua kisu wanachotumia kwenye shughuli zao za mapishi kilichokuwa ndani ya vyombo na kumchoma kifuani.

Tadei alianguka chini na jitihada za wafanyakazi wenzake za kumwahisha hospitalini zilishindikana baada ya kufa muda mfupi.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi kukamilika.

ZeroDegree.
Auawa kwa kuchomwa kisu akigombea soda. Auawa kwa kuchomwa kisu akigombea soda. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2016 11:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.