Loading...

Wahamiaji haramu mkoani Kagera kusakwa mtaa kwa mtaa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu. 
Wahamiaji haramu waliojificha mkoani Kagera sasa wataanza kusakwa mtaa kwa mtaa na kitongoji kwa kitongoji.

Hatua hiyo inatokana na Serikaki mkoani humo kuamua kuchukua hatua madhubuti kudhibiti wahamiaji haramu, kukabiliana na biashara ya magendo, uhalifu na vitendo vya ukatili.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu amesema hayo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka akihitimisha ziara ya siku nne mkoani humo.

Amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na baadhi ya wataalamu watapita kila kijiji na kitongoji kubaini nani ni raia na yupi ni mhamiaji haramu ili watakaobainika kuwa wageni walioingia mkoani hapa bila vibali vya uhamiaji wachukuliwe hatua za kisheria.

“Aliye na kibali halali cha Idara ya Uhamiaji kamwe hatasumbuliwa, bali wale walioingia kupitia njia za panya na badhi yao kujihusisha na uhalifu na biashara ya magendo,” amesema Kijuu.

Amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya mipakani kama vile wilaya za Karagwe, Missenyi na Kyerwa kuacha kujihusisha na biashara za magendo na hasa ya kahawa nchini Uganda badala yake wafuate utaratibu na sheria.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Yahya Kateme amesema wataendelea kuwa karibu na watendaji wa Serikali kwa masilahi ya nchi na kuhimiza uzalendo bila kujali itikadi za kisiasa.

“Tutakwenda sambamba na watendaji wa Serikali, tukikosoa kwa hoja na ushahidi na kusifu wanaowajibika,” amesema Kateme.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Wahamiaji haramu mkoani Kagera kusakwa mtaa kwa mtaa. Wahamiaji haramu mkoani Kagera kusakwa mtaa kwa mtaa. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2016 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.