Serikali yatangaza kiama kwa waliogushi taarifa zao ili kupata mikopo ya elimu ya juu.
Waziri wa Elimu, Dkt. Joyce Ndalichako. |
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Simon Msanjila, wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must). Alisema taarifa ya suala hilo imefika wizarani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Simon Msanjila. |
Alisema wizara inashughulikia suala hilo kwa kuanza uchunguzi wa kila mwanafunzi aliyepata mkopo kwa wanachuo wote.
Msanjila alisema mwanachuo yeyote atakayebainika kutoa taarifa za uongo ili kupata mkopo, Sheria itachukua mkondo wake, ikiwamo kufikishwa mahakamani ili kurejesha gharama zote.
Aidha, aliwatoa hofu wanafunzi waliokosa mkopo katika vyuo mbalimbali kuwa suala la mikopo linatolewa kwa awamu na kwamba kama wanasifa stahiki lazima wapate mkopo.
ZeroDegree.
Serikali yatangaza kiama kwa waliogushi taarifa zao ili kupata mikopo ya elimu ya juu.
Reviewed by Zero Degree
on
12/28/2016 11:27:00 AM
Rating: