Loading...

Azam yamtupia virago kocha Hernandez pamoja na wasaidizi wake wote.

UONGOZI wa klabu ya soka ya Azam umemtupia virago kocha wake Mhispania Zeben Hernandez baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya kwenye Ligi Kuu.

Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 27, timu hiyo haina mwenendo mzuri tangu kuanza kwa msimu huu na licha ya usajili iliofanya bado imekuwa haipati matokeo ya kuridhisha.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Azam zilizopatikana jana jioni zilisema Hernendez pamoja na wasaidizi wake wote kutoka Hispania wametupiwa virago.

Taarifa zaidi zinadai kati ya Kalimangonga ‘Kally’ Ongala au Hans van Pluijm ndio watakaopewa mikoba kuiongoza timu hiyo ambayo mmiliki wake anafanya uwekezaji mkubwa.

Kally kwa sasa ni kocha wa Majimaji aliyeanza kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa raundi ya kwanza baada ya kuwa haipati matokeo mazuri.



Kocha huyo aliwahi kuwa msaidizi Azam chini ya Muingereza Stewart Hall alioifundisha timu hiyo kwa mafanikio. Pluijm kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, nafasi aliyoianza hivi kwenye mzunguko wa pili baada ya nafasi yake ya ukocha kuchukuliwa na Mzambia George Lwandamina.

Pluijm aliifundisha Yanga kwa mafanikio ngazi ya kitaifa na kimataifa, amekuwa akitajwa kwenda Azam tangu mwishoni mwa raundi ya kwanza ya ligi.

Katika msimu huu, Azam imecheza mechi 17 ikishinda saba, kupoteza mechi nne na kutoka sare mechi sita. Hata hivyo msemaji wa Azam Jaffar Iddi hakukataa wala kukubali taarifa hizo zaidi ya kusema hawezi kuzizungumzia jana na kuahidi angezungumza na waandishi wa habari leo.

ZeroDegree.
Azam yamtupia virago kocha Hernandez pamoja na wasaidizi wake wote. Azam yamtupia virago kocha Hernandez pamoja na wasaidizi wake wote. Reviewed by Zero Degree on 12/29/2016 11:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.