Loading...

Fabregas aipasha Chelsea kileleni kwa alama 6 zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL].

Fabregas amefunga magoli mengi dhidi ya Sunderland (matano) hii ikiwa ni zaidi ya timu yoyote kwenye EPL aliyokutana nayo.
Chelsea wameweka pengo la alama sita na kuendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu soka England baada ya goli alilofunga kiungo Cesc Fabregas kipindi cha kwanza kuwa pekee na la ushindi.

Fabregas alipachika goli hilo kwa ufundi wa hali ya juu kwa kuupeleka mpira kwenye kona ya kushoto ya lango la Sunderland baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Willian na kuwa ushindi wa kumi mfululizo kwa Chelsea.

Ulikuwa ni ushindi muhimu sana kwa Chelsea baada ya Arsenal kuteleza siku ya Jumanne kwa kuchapwa 2-1 na Everton na hii inamaanisha vijana wa Antonio Conte watakuwa kileleni mwa ligi hiyo kwa msimu huu wa Christmas.

Matokeo ya michezo mingine

  • Middlesbrough 0-3 Liverpool
  • West Ham 1-0 Burnley
  • Crystal Palace 1-2 Manchester Utd
  • Manchester City 2-0 Watford
  • Stoke city 0-0 Southampton
  • Tottenham Hotspur 3-0 Hull City
  • West Bromwich Albion 3-1 Swansea City
ZeroDegree.
Fabregas aipasha Chelsea kileleni kwa alama 6 zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]. Fabregas aipasha Chelsea kileleni kwa alama 6 zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]. Reviewed by Zero Degree on 12/15/2016 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.