Loading...

Fellaini aomba kuondoka Manchester United.

HII inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Manchester United zaidi ya usajili wa beki Victor Lindelof anayetarajiwa kutua klabuni muda wowote kuanzia sasa.

Unajua ni habari gani hiyo? Imeripotiwa kuwa kiungo Marouane Fellaini amewaambiwa wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka United na kujiunga klabu za Jiji la Milan, Italia.

Kiungo huyu wa kimataifa wa Ubelgiji amepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza na inaaminika ameanza mazungumzo na AC Milan.

Kwa mujibu wa jarida la The Times, Fellaini amechukizwa na kitendo cha mashabiki wa United kumzomea kila anapotaka kuingia uwanjani hali inayomfanya atamani kuachana na klabu hiyo wakati dirisha dogo la usajili, Januari mwakani litakapofunguliwa.

Inadaiwa mapumziko aliyokwenda katika Jiji la Milan yalikuwa ni kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa klabu za Inter na AC Milan ili kujua ni wapi penye maslahi mazuri kwake.

ZeroDegree.
Fellaini aomba kuondoka Manchester United. Fellaini aomba kuondoka Manchester United. Reviewed by Zero Degree on 12/21/2016 12:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.