Loading...

Habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu Santi Cazorla.

Kama ni shabiki wa timu ya Arsenal ya England ni dhahiri kwamba hutafurahishwa na habari zilizoripotiwa December 1 2016 kuhusiana na kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea timu hiyo Santi Cazorla.

Taarifa kutoka BBC zinaeleza kuwa Cazorla atafanyiwa upasujai wa kifundo cha mguu (enka), upasuaji ambao utamfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu, kiungo huyo hajaichezea Arsenal toka katikati ya mwezo October baada ya ushindi wa Arsenal wa goli 6-0 dhidi ya Ludogorets mchezo wa UEFA.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Cazorla msimu uliyopita alikosa kuichezea Arsenalkwa miezi saba, kutokana na kuwa na jeraha la goti, Cazorla ambaye ameichezea Arsenal mechi 11 na kuifungia magoli mawili katika mashindano yote msimu huu, atafanyiwa upasuaji Sweden wiki ijayo.


ZeroDegree.
Habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu Santi Cazorla. Habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu Santi Cazorla. Reviewed by Zero Degree on 12/02/2016 03:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.