Loading...

Mwanamke adaiwa kumchinja mtoto mchanga.

POLISI wamemkamata na kumfikisha mahakamani mwanamke kwa tuhuma za kumuua mtoto mchanga kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Hassan Momba, imedaiwa na upande wa mashitaka kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 25, mwaka huu.

Aliyepandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kuua kwa makusudi ni Mariam Nyanza ( 43 ), mkazi wa kata ya Azimio, wilaya ya Urambo, mkoani Tabora.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Philibert Pimma, amedai kuwa siku hiyo mshitakiwa alimuua kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili mtoto mchanga wa Hadija Juma.

Pimma amedai kuwa siku hiyo saa 2:00 asubuhi kwa makusudi mshitakiwa Mariam alimuua mtoto huyo alipokuwa akimsaidia mama yake kujifungua ndipo akatenda unyama huo.

Mwendesha mashitaka aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa akiwa kama jirani wa Hadija kwa makusudi na kwa kutumia kitu chenye ncha kali alitenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtoto mchanga.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo kwani shauri lake litasikilizwa na Mahakama Kuu, hivyo kesi hiyo imepangwa kutajwa Desemba 8, mwaka huu.

ZeroDegree.
Mwanamke adaiwa kumchinja mtoto mchanga. Mwanamke adaiwa kumchinja mtoto mchanga. Reviewed by Zero Degree on 12/02/2016 03:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.