Loading...

Jeshi la Polisi kutoa msimamo wake leo dhidi ya kauli ya Mzee wa Upako.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki tatu mfululizo akijibu yaliyoandikwa na vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani yake.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatoa ufafanuzi leo.

Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Jeshi la Polisi kutoa msimamo wake leo dhidi ya kauli ya Mzee wa Upako. Jeshi la Polisi kutoa msimamo wake leo dhidi ya kauli ya Mzee wa Upako. Reviewed by Zero Degree on 12/13/2016 01:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.